Rais aliyetolewa madarakani nchini misri pamoja na viongozi wengine 14 wa Harakati ya
Ikhwanul Muslimin, watashtakiwa kwa kosa la kufanya mauaji ya umati
nchini humo.
RAIS Mwenyewe |
Rais huyo wa zamani wa Misri atapandishwa kizimbazi, kujibu mashtaka ya mauaji ya watu saba wa
upinzani waliouawa katika maandamano ya tarehe 5 Desemba mwaka jana.
Miongoni mwa viongozi 14
wanaotajwa kujibu shitaka hilo ni pamoja na Makamu
Mwenyekiti wa chama cha Uhuru na Uadilifu tawi la kisiasa la Ikhwanul Muslimiin
nchini Misri .
Zaidi ya watu 1000 wamekwishauawa na zaidi ya
viongozi 2000 wa Harakati ya Ikhwanul Muslimiin kutiwa mbaroni, tangu jeshi la
nchi hiyo lilipochukua hatua ya kumuondoa madarakani rais Muhammad